Kama unajijua huna ubavu wa kumuacha mtu hembu acha kutingisha Kiberiti, kila saa kusema “Kama vipi bora tuachane!” Watu wengi wenye katabia haka wanajiona kama keki wana kwamba hawawezi kuachika lakini wengi wao huishia kuumia tu kwani mwisho wa siku wao si keki na hao wanaoambiwa nao huchoka ipo siku wataamua kuondoka.
Kumbuka kuwa mapenzi ni kama nyumba ya kupanga hivyo kama wewe ni mmiliki wa nyumba kila siku kazi nikuwatishia wapangaji wenzako kwa kuwaambia “Kama mmeshindwa mashariti basi bora muondoke!” Jua kabisa kuwa mpangaji yeyote mwenye akili ataanza kutafuta nyumba nyingine yenye amani zaidi ya hiyo yako.
Hivyo kama ulikua unatingisha Kiberiti basi jua ipo siku wataondoka kweli na utabaki kulialia njaa, kuna nyumba nyingi huko mtaani na yako haina upekee wowote. Kuna siku huyo unayemtishia “Bora tuachane!” atakuacha kweli na kwa bahati mbaya sana watu wenye tabia hii huwa hawana ubavu wa kuacha, mtu mwenye ubavu wa kuacha huwa hatangazi, unasatukia tu kashaondoka au hapatikani!
Hawa wakulia lia wengi huwa hawana ubavu wa kuacha, hutumia kitisho hicho kama kuonyesha kuwa wao ndiyo wenye nguvu katika mahusianao ingawa kiuhalisia katika mioyo yao wanalia kama kibinti cha chekechea kilichonyimwa kwenda shule na viatu vipya. Kama unatabia hii badilika ipo siku huyo unayemtishia atakuacha si kwakua hakupendi bali kwakua kachoka kutishiwa kuachwa!
Lakini kama uko kwenye mahusiano na mtu wa namna hiyo, jipange kuondoka wakati wowote kwani watu wasiojiamini ni kama ‘wehu’ flani hivi, anaweza kukuacha tu kwa muda ili kukupima kama utamnyenyekea au la? Anaweza kutafuta mtu mwingine na kukuonyesha ili tu umuone yeye ni kidume au mwanamke kweli! Nilazima ifikie hatua useme imetosha kama ni kuniacha niache niende,hakikisha unajilinda kiuchumi kwani hawatabiriki!
EmoticonEmoticon