Unapomfumania mume wako una machaguo mawili tu, narudia una machaguo mawili tu. Chaguo la kwanza ni kuondoka na kuachana naye, kuamua kusema siwezi kuishi na mwanaume anayechepuka na kuondoka na chaguo la pili ni kubaki na kusamehe, kuacha kuuzungumzia huo mchepuko wake, kuacha kumfuatilia na kubwa kabisa kuacha kuwa na kisirani kabisa. Hakuna chaguo la tatu la kubaki na kuendelea kulalamika au kuwa kisirani!
Wanawake wengi wanabaki, najua ni ngumu kuondoka, wanabaki iwe ni baada ya kuombwa msamaha wa uongo au hata msamaha wakweli. Lakini wakishabaki sasa kila siku atakua anatajwa huyo mwanamke mwingine. Akichelewa utasikia ulikua kwa huyo Malaya wako, akipokea simu ulikua unaongea na flani. Akirudi kashiba utakua umekula kwa huyo flani.
Kwakifupi kila kitu kinakua huyo flani kiasi kwamba mwanaume hata kurudi nyumbani anawaza mara mbili. Niwaambie tu dada zangu wanaume hatupendi kelele, kisirani na mara nyingi hata kama kweli mwanaume anachepuka na bado hajamuacha huyo mwanamke lakini kama akirudi nyumbani kila siku nikukumbushiwa kuhusu huyo mwanamke basi huona bora kurudi na kwenda kule kwenye amani kuliko kuvumilia kelele za mke.
Kama umechoka, kama hutaki, si uondoke, unabaki halafu unaanza kupigia watu kelele kila siku, kununia watu mwanaume unarudi nyumbani mtu kanuna kisa tu alikufumania mwaka jana! Narudia wanaume wengi hata kama wao ndiyo wamekosa lakini kama umemaua kusamehe na unakumbushia makosa kila siku ni bora arudi kwa mchepuko.
Kwanza huo mchepuko wake ushajua kua wenyewe ni mchepuko hivyo akichelewa, asiporudi, asipopokea simu na hata asipokula hakuna kele eti ulikua kwa mkeo! Hivyo mwanaume huona bora aende huko ambako hakuna kelele. Sasa wewe samehe halafu kila siku umenuna, kila siku ni kelele huyo mwanamke haondoki midomoni mwenu jua kua hata kama umeamua kubaki mume atakutelekeza na utaishia kulia kila siku, kama umeamua kusamehe, samehe na nyamaza acha kusumbua watu!
EmoticonEmoticon