Monday, May 18, 2020

MAISHA YA SASA TUNAHITAJIANA SANA HATA TUNAVYOHITAJI VITU VINGINE

Tags


Maisha ya sasa tunahitajiana sana kuliko hata tunavyohitaji vitu vingine. Upendo na kufarijiana kwenye hii dunia iliyotawaliwa na hofu ni muhimu sana ili kuhakikisha maisha yetu yanakua yenye maana.
Sio tuu ukaribu uwepo kwa wapenzi bali hata familia bila kusahau ndugu jamaa na marafiki.
Hatuishii hapo bali lazima tutambue kuna wenye nacho na wasio nacho hivyo lazima tusaidiane na tutambue kwamba sisi ni wamoja na tunaishi kwa uwezo wa aliye tuleta dunia tutimize matakwa yake.
Sio mwingine bali ni Mungu mkubwa wa ulimwengu hivyo basi tuendelee kumshukuru na kumuomba sababu yeye muda sio mrefu atatuvusha kwenye janga linalotukabili na maisha yataendelea kama kawaida na hata kuwa bora zaidi.
Tuishi katika upendo aliotuagiza yeye na tutambue kwamba Mungu ni mwema kila wakati.
Nawatakia Jumapili Njema.
Share
Like Page



EmoticonEmoticon