Sunday, May 17, 2020

MAMBO YA KUKUSAIDIA KUONGEZA NGUVU, HAMASA NA FURAHA KATIKA TENDO LA NDOA KWA WANANDOA.

Tags


> Kamwe kusiwepo na dharau baina yenu, mmoja asimdharau mwingine kwa chochote.
> Unachotaka kutendewa, kuwa tayari kumtendea mwenzako tena kwa furaha na upendo.
> Usafi uongezeke baina yenu, sio tu kwenye maeneo ya nje tu bali kwenye miili yenu pia
> Mavazi na mikao yenu “pose” iwe ya kuhamasisha tendo la ndoa nasio kukatisha tama, hapa wanawake wanahusika zaidi.
> Kuweni tayari kujifunza na hata kugharamia mazingira husika ili kuongeza hamasa zihusuzo tendo la ndoa.
> Miili yenu na muonekano wa kila mmoja wenu uwe wa kuvutia na kuhamasisha tendo la ndoa na sio wa kukatisha tamaa katika zoezi hili, hapa namaanisha ukubwa wa mwili, uzito wa mwili na kitambi. Vitambi na miili mikubwa sana ni tatizo katika kulifurahia tendo la ndoa kwa wengi (hapa hakuna cha kujitetea, ukweli ndio huo)
> Jifunze kula na kunywa vitu vipasavyo na vyenye afya, sio kila kitu kwako ni chakula na kinywaji, kuwa na kiasi. Kuna uhusiano mkubwa baina ya vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa na tendo la ndoa.
> Epukeni msongo wa mawazo “stress” kwasababu huathiri sana tendo la ndoa
> Jifunzeni kuiombea “kuifanyia sala” hali yenu ya tendo la ndoa na pia kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo nzuri baina yenu, maana ni mpango kamili wa mungu kwa wanandoa kufurahia tendo la ndoa. Ninauhakika kabisa kama unafanya tendo hili kwa wizi huwezi kujaribu kumshukuru Mungu.
> Zishuhulikieni hofu na maumivu yenu ya ndani ya moyo “internal pains”, msijaribu kuzifunika kanakwamba hazipo, kwasababu zitakapolipuka zitalipua mahusiano yenu pia.
> Zungumzieni kuhusu maumivu na majeraha yenu ya nyuma “past pains” na kumuomba Mungu awasaidie kupona.
Share
Like Page



EmoticonEmoticon