Sunday, May 17, 2020

Mara nyingi ukiona mwanamke anakuambia bora tuchane, lakini baada ya muda anataka mrudiane!

Tags

Mara nyingi ukiona mwanamke anakuambia bora tuchane, lakini baada ya muda anataka mrudiane! Yaani kila mkiogomba kidogo anakuambia bora tuachane, wewe unaishia kuomba misamaha mingi tena kwenye makosa ambayo hata hayana kichwa wala miguu. Labda kama unampiga, labda kama wewe ni Malaya kila dakika anakufumania, kama ni hivyo wewe hapa huhusiki.
Lakini kama wewe si Malaya, ila kuna makosa kidogo kidogo kama kuchelewa kupokea simu, kama kakuomba pesa umesema huna au umemuambia nitakupa ukakosa, umemuambia mkutane sehemu ukachelewa, yaani vitu vya kijinga jinga tu anakuambia bora tuachane. Ndugu yangu, huyo mwanamke ana mwanaume wake mwingine.
Yuko na wewe kwakua labda unamhudumia vizuri na huyo jamaa yake ni mpare hatoi chochote, ana jamaa yake mwingine ambaye ni Malaya sana na hamuelewi hivyo anashindwa kuamua kuwa na wewe ambaye unampenda sana na kumnyanyeke kama amebeba benki tumboni. Anaamani kukuacha na atakuacha, lakini hajapata mtu anayemsisimua au mtu ambaye atabeba majukumu yako.
Mara nyingi wanaume wanaoambiwa hivi ni wale ambao wanajua sana kutoa pesa, lakini wakishindwa kutoa kidogo tu wanaambiwa kuhusu kuachwa, mara nyingi ni wale wanajali mpaka wanaboa, kila dakika anapiga simu, akichelewa kupokea anaambiwa bora tuachane. Wale wanaume vichomi wale, wale Malaya wa kufa mtu ni ara chache sana kuambiwa, mwanamke hasemi kwakua anajua kuwa msela hatishiwi nyau!
Kwa maana hiyo, ndugu yangu, kama mwanamke wako humpigi, humtukani, humnyanyasi lakini kila kakosa ni bora tuachane, basi mpe bora tuachane mbili. Ya tatu, akisema hivyo usiongee kitu, usiombe msamaha, kusanya vitu vyake, vyote mkabidhi muambie kwa heri. Muache aondoke, hata kama unampenda vipi, kama akikaa mwezi hajakutafuta basi nipigie simu unishukuru kwani ulishaachwa tangu mwaka jana ila ulikua unatumika tu kama mtu wa dharura kwamba nikikosa mume hata huyu anafaa.
Yaani wewe ni wale ambao wapare tunasemaga “Bettrer half shari than Full Shari” kwa ndugu zangu wa Machame ambao hamajambulia kitu namaanisha “Bora nusu shari kuliko shari kamili!” yaani alikua na wewe kwaajili ya kukutumia kwa matumizi ya kiume wakati akitafuta mwanaume. Huna haja ya kumtafuta, rudi nyumbani, lia, omboleza na omba upate wa namna yako!


EmoticonEmoticon