Sunday, September 20, 2020

Wahitimu wa mafunzo ya JKT operesheni uchumi wa kati 2020 watakiwa kuepuka vitendo vya kihalifu

Tags

 


Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) kwa mujibu wa sheria kupitia operesheni uchumi wa kati 2020 katika Kikosi cha Jeshi namba 843 kilichopo wilayani Nachingwea, mkoa wa Lindi wameonywa wasitumie vibaya ukakamavu waliopata kutokanana mafunzo hayo.


Onyo hilo lilitolewa jana wilayani Nachingwea na kanali Philipo Mahende wakati wakufunga mafunzo kwa vijana waliojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria operesheni uchumi wà kati 2020 katika Kikosi cha Jeshi namba 843(843KJ).


Kanali Mahende ambaye alizungumza katika ufungaji huo wa mafunzo kwaniaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Jenerali Charles Mbuge alisema vijana hao waliomaliza mafunzo hawanabudi kutumia mafunzo hayo kutatua changamoto za maendeleo kwa maslahi ya taifa na katu wasitumie mafunzo hayo ambayo yamewafanya kuwa wakakamavu kufanya vitendo vya uhalifu ambavyo ni uvunjaji wa sheria.


Alisema vijana hao wanajukumu na wajibu wa kubadilisha fikra na mtazamo hasi wa baadhi ya vijana wanaodhani JKT ni eneo la kutesea vijana. Mtazamo ambao umesababisha baadhi ya vijana waliotakiwa kujiunga ili wapate mafunzo hayo hawakujiunga. Kwahiyo wameshindwa kupata mafunzo hayo muhimu kwao na taifa kwa jumla.


" Waambieni JKT siyo sehemu ya mateso, bali ni sehemu ya kujifunza mambo mbalimbali na muhimu na mazuri kwenu nyinyi vijana binafsi na taifa kwa jumla," alisisitiza kanali Mahende.


Kamanda Mahende aliwaasa vijana hao wafanyie kazi kwa vitendo mafunzo waliyopata ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini kwakutumia fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawasaidia kufikia na kutimiza azima yao ya kujikwamua kutoka kwenye umaskini.


Ofisa huyo wa Jeshi alionya kwamba kushindwa kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na taifa kunaweza kuwaingiza kwenye kundi la watu wanaolalamika maisha magumu na kuilamu serikali muda wote. Wakati ukweli nikwamba wakitumia mafunzo hayo, licha wao wenyewe kunufaika lakini pia watakuwa ni mfano kwa vijana wenzao na jamii kwa jumla.


Kwaupande w ake mkuu wa Kikosi(C.O) wa  843 KJ,  Luteni Kanali Nyagalu Malechela alisema vijana waliohitimu mafunzo hayo walitakiwa kuwa 987. Kati ya hao vijana 727 ni wavulana na 260 ni waschana. Hata hivyo vijana 17 hawakufanikiwa kumaliza kutokana na sababu mbalimbali. Ikiwamo utoro na magonjwa.


Kamanda Malechela alisema katika mafunzo hayo ambayo yalianza tarehe 3.09.2020 wahitimu hao walijifunza mambo mbalimbali ambayo baadhi ya hayo ni mbinu za kivita,ujanja wa porini,usomaji wa ramani,silaha ndogo ndogo,kwata, sheria za kijeshi,uraia, utimamu wa mwili, mazingira, mabomu ya mkono, uokoaji na ugonjwa wa UKIMWI.


Alisema masomo yote hayo yalilenga kuwajengea uwezo ujasiri,uvumilivu, ukakamavu, uraia na ulinzi wa nchi. Lakini pia vijana hao walihudhuria warsha na semina fupi  wakiwa hapo. Kwamfano tarehe 17.08.2020 walipata elimu kutoka tume ya vyuo vikuu ya jinsi kutuma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu.


Kamanda Malechela pia alisema wahitimu hao walifundishwa kuhusu elimu mbambali. Ikiwamo za kibenki na kupambanana Rushwa kutoka kwa maofisa wa taasisi hizo. Lakini pia katika mwezi huu wa Septemba, tarehe Mosi, mwaka huu wa 2020  walijitolea kuchangia damu.


Aidha alisema muda wa mafunzo hayo ulitakiwa kuwa wa miezi mitatu. Hata hivyo kutokanana kuzuka tatizo la ugonjwa wa homa kali ya mapafu( Covid-19) unaosababishwa na virus vya Corona yalichelewa kuanza. Ugonjwa ambao kwasasa umetokomea na haupo tena hapa nchini.


EmoticonEmoticon