Thursday, May 7, 2020

UTOFAUTI MKUBWA KATI YA KUMVUMILIA MPENZI WAKO NA KUPOTEZA MUDA WAKO KWAKE!

Tags


Natamani sote ifikie wakati tujitambue, na kuelewa kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya kumvumilia mpenzi wako, na kupoteza muda wako kwake.
Mtu anayejitambua anaelewa uvumilivu ni pale unapokuwa tayari kuyabeba mazito, madhaifu, makosa, na mapungufu ya mpenzi wako.
Pamoja na kukubali kuwa nae katika kila kipindi kigumu ambacho wote mnapitia bila kujali maslahi yako binafsi.
Lakini hii ni kwa yule mtu anayekupenda, anakujali na kutambua kuwa wewe ndiye wake wa maisha.
Na naomba utambue kuwa kupoteza muda, ni pale unapoamua kumvumilia mtu asiyekupenda, wala kukujali.
Kumng'ang'ania mtu asiye na malengo na wewe.
Kumlilia mtu asiyejua uchungu na thamani ya machozi yako.
Kujiwekea matumaini kuwa utamuoa au utaolewa nae, wakati yeye miaka inakatika hana dalili ya kutaka kukuoa au kuolewa na wewe.
Na matendo yake yanaonyesha wazi kuwa hana mapenzi ya dhati kwako.
Jitambue, ijue thamani yako.
Huu sio mwaka wa kukubali kupotezewa muda na mtu asiye na malengo na wewe.
Najua inauma, na ngumu kumuacha aende lakini kumbuka future yako ni muhimu kuliko chochote.



EmoticonEmoticon