Thursday, June 4, 2020

MWANAMKE KATAA KUWA MPENZI KUBALI KUWA MCHUMBA*

Tags

*MCHUMBA* Ni mtu yule aliyeaminiwa na mwanamke au mwanaume kuwa huyu anafaa kuwa mke au mume siku za usoni na akakubalika kwa wazazi pande zote mbili kwa utambulisho rasmi kwa ndugu jamaa marafiki kanisa na jamii kwa ujumla
*MPENZI* ni mtu aliyependa mtu au kitu kwa tamaa fulan aidha kuwa nacho milele ama baada ya muda mfupi kukiacha na kupenda kingne
*UCHUMBA* Ni utambulisho wa matokeo mazuri ya mahusiano ya mpenzi na mpenzi ni hatua njema ya ndoa ni picha ya upendo wa kweli
*ZIFUATAZO NI HASARA ZA KUWA MPENZI MUDA MREFU*
*Hasara No1. KUOLEWA NI NDOTO*
Dada chunga sana kuwa mpenzi kwako kuolewa itakuwa ni ndoto maana ukiwa mpenz kwa Muda mrefu kuna mambo ambayo huwa yanapunguza morali ya mwanaume kukuhitaji tena na kukuona sasa kama ni mtu wa kawaida kama wengne na kufanya kupunguza upendo wa kweli na kukuona umeshuka bei sio special tena ni mtumba usio na thamani
*Hasara No2: KUWA CHOMBO CHA STAREHE*
kwa kizazi hiki nmeona hata waliokoka nao wanashiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa leo hii makanisani pamekuwa kama sehem ya kupatia wachumba Dada usikubali Kuwa mpenz ukatumiaka kama chomba cha kupunzia stress kwa mwanaume
*HASARA NO 3. KUSHUKA THAMANI NA UBORA*
baada ya kutumika kama chombo cha starehe jua lazma tu utashuka thamani mwanaume atakuona kama nyanya iliyooza hata tamani tena kuitumia kwa maana ubora umepungua sio kama ilivyokuwa mbichi, mwanaume atakuona huna thaman tena maana hakuna asichokijua kwako sasa akuoe ili agundue nini tamaa yake ameshaimaliza hapo ndio utaanza kuona dharau ambazo hukuzitegemea utajiuliza sana kweli huyu ndio yule aliyekuwa ananipigia goti kuniomba niwe mpenzi wake?
*HASARA NO 4. KUPATA MARADHI*
ogopa sana kuwa na mpenzi kizazi hiki kimeharibika sana magonjwa yametawala mnoo hasa janga la UKIMWI limeshamiri sasa kwa kasi kubwa ukikubali kuwa mpenz aisee utakutana na dhahama hili la magonjwa maana mpenzi usidhani upo pekee ako magonjwa ya zinaaa yatakumaliza mwanamke ogopa sana kuwa mpenz na kubali kuwa mchumba ili kumnyima uhuru mkubwa mwanaume wa kuwa na mpenz mwingine kama akiwa Mpenzi tu kwako atakuwa na uhuru wa kuwa na wapenzi wengi na kukuleteamagonjwa
*HASARA NO 5. KUJIFUNGULIA NYUMBANI*
hii sasa imekuwa ni kilio kwa wanawake wengi baada ya kuwa na wapenzi wao kwa muda mrefu wamewazalisha na kuwatelekeza majumbani mwao na watoto wao. Mdada usikubali kuwa na mtoto asiye na baba kwa kukubali kuwa na mpenz kwa muda mrefu mapenzi mapenzi ni kama upofu muda wowote unaweza ukaanguka shimoni na ukaumia pekee yako uliyemtegemea akakukimbia na kukucha shimon bila ya msaada
*FAIDA ZA KUWA MCHUMBA*
*FAIDA YA 1. UHAKIKA WA KUOLEWA*
japo sio wote walio wachumba wanaweza kuolewa la hasha ila mara zote aliyemchumba huwa anauhakika wa asilimia 95 za kuwa mke wa mtu maana mwanaume tayari ameshajifunga mwenyewe kutangaza na kukubaliana na wazazi wote Amekuchagua wewe kuwa mke wake mtarajiwa kwa hiyo unafaida ukiwa mchumba wa mtu
*FAIDA YA 2. KUWA NA HESHIMA*
Hata wale wanaume wasio na adabu wataanza kuwa na heshima maana sasa umekuwa mchumba wa mtu hawatakusumbua tena. Pia utapata heshima kwa wazazi na ndugu zako nao watajiskia vizuri kwa hatua hiyo uliyoifkia, jamii pia itakupa heshima maana kuna watu hata hatua hiyo hawajaweza kuifikia kabisa
*FAIDA YA 3.MOYO KUTULIA*
Wakati wengne wanatenganisha mavi ya panya kwenye unga wa ugali wewe sasa umeshatenga maji ya ugali umepika umetenga unasubiri kula huna mashaka tena ukiwa mchumba moyo hauwez kuhangaika tena kujiuliza nitaolewa na nani moyo utatulia kabisa maana uhakika unao wa kuitwa mke wa mtu
*FAIDA YA 4. KUKUA KIAKILI NA FIKRA*
Hapa sasa wanawake wengi ndio huanza kujifunza jinsi ya kuishi na mwanaume akili yake sasa hupanuka na fikra zake hufikiria namna ya kuishi na mwez wake,huu ndio muda mzuri wanawake huacha utoto na ukubwa kuingia kukua kimawazo kifikra na kimazingira pia
*FAIDA YA 5. KUPATA JINA NA SIFA NJEMA*
Hata kama ulikuwa na tabia mbaya mtaani kwako ila ukifka hatua ya uchumba wale wale waliokusema ndio wakwanza kukusifia tena "umeona fulan katulia hadi kapata mchumba sasa ataolewa mwezi ujao" wakat hao hao kipnd cha nyuma walisema huto olewa mwanadamu ni mwanadamu tu siku zote ila kuwa MCHUMBA wa mtu kunaleta sifa njema hugeuza giza lililokuwa limekufunika kuwa nuru
*HITIMISHO* huwezi kuwa mke wa mtu wa mtu kabla hujawa 1.mpenzi 2.mchumba kisha 3. mke lazima upitie hatua tatu hizo ili uwe mke wa mtu TAHADHARI mwanamke usikubali kubaki kwenye hatua ya kwanza kuwa mpenzi hiyo ndio steji mbaya sana ambapo ukikubali kubaki kuwa mpenzi itakula upande wako hapo ndio utakutana na *Uchungu,streess,majuto,kujilaani na kulaumu* usikubali kataa kamwe kuwa mpenzi kama unahitaji kupiga hatua nyingine kataa kuwa mpenzi kubali kuwa mke mtarajiwa yaani MCHUMBA maana hata mtoto anapozaliwa huanza kukaa kutambaa na mwisho kusimama MWANAMKE usikubali kabisa kukaa milele hakikisha unasimama ukiona MWANAUME anataka ukae tu hataki kukusimamisha kuwa mchumba kwako jua huyo hajatokana na Mungu kabisa MWANAMKE Shituka acha kufanywa kama keki kila mtu anaonja kama tamu ukimuendekeza mwanaume kukufanya mpenzi tu hakika hutafikia malengo ya kuwa mke wa mtu utabaki kama daladala kila mtu atapanda mwisho wa siku itaharibika itakaa garage tu utabaki kuchezewa tu utazeekea kwenu bila matokea yoyote MWANAUME sio mtu wa kumuonea huruma kabisa eti unampa kila kitu utajuta one day MWANAMKE TAFAKARI CHUKUA HATUA


EmoticonEmoticon