Thursday, June 4, 2020

ACHA MANENO YA SHOMBO MUME WAKO SI SHOGA YAKO MNAYEGOMBANIA BWANA!

Tags

Shida moja ya wanawake nikuwa, ukimuonyesha kuwa unampenda sana, unamsikiliza na kila dakika wewe ni kumuomba msamaha hata kama kosa si lako basi anataka kukukalia kichwani. Ukiwa mpole kidogo na ukapenda amani basi anataka kuongea na sauti yake kusikika, anataka kuwa mwanaume kwenye nyumba.
Unakuta mwanamke mume wake anamhudumia kwa kila kitu lakini haridhiki, mwanaume akishindwa kumpa kitu kidogo tu basi ataongea, si kuongea tu bali anaongea maneno tena yale ya shombo. Utasikia “Mwanaume gani unashindwa hata kuninunulia sare… mwanaume gani Mama yangu anaumwa hata nauli huwezi kunipa… kwenye gari hili nalo gari… hivi katika nyumba hii nayo nyumba au kibanda tu… wanaume wenzako hivi na vile…”
Haya maneno yanaboa na hata kama mume wako ni malaika basi jua kuwa ni rahisi kukuchoka. Tena unakuta anaongea maneno ya chombo namna hii lakini hana kitu, unamhudumia yeye na ndugu zake ila bado anaona kama haitoshi. Dada yangu, kama umepata mwanaume wa namna hii, hafanyi makubwa lakini angalau anakupenda na kukuhudumia acha maneno ya shombo.
Jifunze kushukuru, kuna wanawake wenzako huko mtaani mwaka wa kumi sasa, hajawahi hata kuvaa chupi aliyonunuliwa na mume wake ila wewe unalalamika kisha kashindwa kukupa hela ya Kikoba! Aisee mnaboa, huyo mwanaume wako ni matoleo ya zamani, yaani huyo mwanaume unayemtaka hata mimi ninayeandika hapa siko hivyo, hivi ndiyo mke wangu anijibu hivyo, aisee atashangaa amelala kwangu ila anaamkia kwao Mama yake anamuuliza vipi tena?
Dada maisha ni magumu, mumeo anapohangaika kuhakikisha chakula kipo mezani hembu basi shukuru kwa chakula ndiyo uombe Gauni. Kama ni rahisi toka utafute wewe tuone. Nishamaliza,



EmoticonEmoticon