Kama ni Mama na una mtoto wako, awe ni wakike au wa kiume, ambaye bado ni mdogo hajajitambua, hakikisha angalau unemuogesha mara mbili kwa wiki. Narudia hakikisha unamuogesga mara mbili kwa wiki, katika kumuogesha angalia vitu vikubwa viwili. Kwanza kabisa angalia sehemu zake za siri, kwa mtoto wa kike angalia nyuma na mbele, narudia angalia nyuma na mbele.
Angalia kwanza kama pamekaa kawaida, kwamba kama pamepanuka sana au la, ngalia kama pana michubuko ya aina yoyote, angalia kama pana mapele ambayo hayaeleweki. Pili angalia michubuko katika mwili wake, makovu na alama nyingine katika mwili wa mwanao ambazo si za kawaida, labda kufinywa, makovu ya kudondoka, kuungua ungua, angalia makovu katikati ya mapaja, angalia makovu katikati ya makwapa na mgongoni.
Watoto wengi wanaonyenyaswa na wafanyakazi, kingono na watu wa kubwa wanakua wanamichubuko, wametanuka na makovu sehemu hizo. Ukiona mwanao ana michubuko isiyoeleweka halafu ukimuuliza anakuambia kuwa alidondoka, alijikata na vitu vingine basi usichukulie poa kabisa, hata kama mwanao ni mtundu kiasi gani chunguza utanishukuru baadaye.
Lakini nimesahau, hakikisha angalau mara mbili kwa wiki unafua au kukagua nguo za ndani za mwanao, hata wewe Baba fanya hivyo kama, kagua nguo za ndani za mwanao, sehemu ya nyuma na mbele, ukiona ukoko mweupe, ukiona damudamu zilizoganda basi ni dalili kuwa mwanao anadhulumiwa kingono. Hata kama upo bieza namna gani unafanya kazi ya kunawisha watu mikono mbinguni, itahitaji nusu saa tu kumjua mwanao.
Hembu #SHARE unaweza kumuokoa mtoto mmoja.
Home
Unlabelled
KAMA WEWE NI MAMA NA UNA MTOTO WAKO AWE WA KIKE AU WA KIUME HAKIKISHA UNAFAMNYIA HILI ANGALAU MARA MOJA KWA WIKI.
Friday, June 5, 2020
KAMA WEWE NI MAMA NA UNA MTOTO WAKO AWE WA KIKE AU WA KIUME HAKIKISHA UNAFAMNYIA HILI ANGALAU MARA MOJA KWA WIKI.
Published on June 05, 2020
Tags
Umezisoma hizi?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon