Friday, June 5, 2020

KUMUAMINI MWENZA WAKO KWA ASILIMIA 100;

Tags

Msingi mkubwa wa furaha katika mapenzi ni kumuamini mwenza wako, kwamba humtilii shaka katika maisha yake, humchungi na wala humfuatilii, kama uko hivyo na unaamini kuwa atafanya maamuzi sahihi ya kulinda mapenzi yenu basi unakua na amani ya moyo na furaha. Lakini kosa kubwa ambalo utalifanya nikumuamini mwenza wako kwa asilimia mia moja.

Kujifanya kipofu na kuamini kwamba hawezi kukuacha, hawezi kukufanyia kitu kibaya, hawezi kukusaliti, hawezi kukudhulumu na mambo hayo. Nikuambie tu ndugu yangu mtu pekee ambaye unapaswa kumuamini kwa asilimia mia moja ni wewe, wengine wote wape asilimia tisini na kumi baki nazo.

Unapomuamini mtu kwa aislimia 100, inakufanya kuwa kipofu, unashindwa hata kuona dalili kua anakusaliti, anakufanyia mambo mabaya. Ni mume wako au mkeo, hajawahi kukuonyesha dalili kuwa anakusaliti, lakini hiyo haimaanishi kuwa hakusaliti, usimchunge lakini jiandae kwa lolote, acha kujipa moyo kuwa hawezi kunifanyia kitu kibaya, anaweza pamoja na upendo wote huo.

Sasa watu wengi wanaoumia hawaumii tu kwa kuachwa, hapana huumia pia katika kuwekeza, mfano mali, kwakua unamuamini mnafanya mambo pamoja, mnajenga katika kiwanja chake au alichoandika jina la Mama yake, mnanunua vitu kwa majina yake na kila kitu kinakua chake. Unamuamini hivyo kama ikitokea akikugeuka hujikuti unapoteza mpenzi tu bali pia unapoteza na kila kitu mlichochuma.

Hapa utaumia zaidi hivyo kama unampenda mtu na yeye anakupenda, hembu muamini kidogo, usijiandae kwa maumivu lakini pia yasikustukize, kwamba jua kuwa huyu sijazaliwa naye hivyo lolote linaweza kutokea. Nikukumbushe tu kuwa hao wote unaowaona wanalia leo, kuna siku walikua wanapendwa kama wewe, yaani walikua wanapendwa kama wewe lakini leo wanalia na hawaamini kama wameachwa hivyo jilinde.



EmoticonEmoticon