Friday, June 5, 2020

KAMWE USIMRUHUSU MTU KUKUPOTEZEA MUDA WAKO MARA MBILI, AKIONDOKA ARUDI KWA MSAHARITI YAKO!

Tags


Kukoseana katika mapenzi kupo na kusameheana kupo pia, nitakudanganya kama nitakuambia usimsamehe mtu ambaye bado unampenda, lakini kama mtu ulikua naye, akauchezea muda wako na kuumiza moyo wako, akaondoka, akirudi basi arudi kwa mashariti yako na si kuuchezea tena moyo wako. Kwamba anaporudi jua yeye ndiyo anakuja kuomba hivyo kama hatakuabaliana na wewe basi muambie kwa heri.
Kwa mfano alikuacha kwasababu ya mwanamke/mwanaume mwingine akirudi muambie kitu cha kwanza ni kauchana na huyo mtu mwingine, yes kukata mawasiliano kabisa hata namba ya simu usiione. Achana na ule ujinga wa oohh sasa hivi tumebaki marafiki tu sijui na nini na nini?
No huo ni ujinga, achana na ule upuuzi ohhh siwezi kumuacha ghafla sijui na nini na nini, kama akikuambia hivyo jua anakuchezea akili yako hivyo muambie Baba/Mama pambana na hali yako tu mimi niko stress free. Kama kuna mtoto basi hayo ni mambo mengine awasiliane kwa mambo mengine si mambo ya kila dakika kila saa No!
Alikua anakupiga, hapokei simu zako na ujinga mwingine, muambie kabisa kuwa kama akikugusa tena nikumpeleka Polisi tu hamna namna na unaweza hata msingizia kesi ya ubakaji au wizi lakini asikuguse tena kama hasira zake bado ni zakaribu basi aondoke akapambane na hali yake!
Lakini kama alikua hapokei simua u hajibu SMS muambie kama bado yupo bize kupokea au kupiga simu basi akamaliza shughuli zake kwanza! Mapenzi ya kuishi sijui unasubiria simu kama unansubiria Arsenal kushinda UEFA huyawezi! Anapaswa kukufanya kipaumbele chake cha kwanza, ajua elikuumiza hivyo hutaki kuumia tena!
Kama alikuchezea miaka mitatu anakuahidi ndoa hajakuoa na kaondoka anakuja kuomba msamaha halafu anajishaua tukae kwanza sijui mchunguzane muambie labda sasa ukampigia X Ray aone ma mifupa yako hivyo kama anarudi ni ndoa na kama hataki akapambane na hali yake!
Ninachosema hapa nikwamba kamwe usikubali ujinga uleule uliowafanya mauchane, kama hawezi kukubaliana na masharti yako mapya basi ni bora msirudiane kwani atakuumiza tena. Alichakuacha au ulimuacha hukufa alipokuacha asasa kwanini akuumize tena kichwa na kukurudishia machungu ya zamani!



EmoticonEmoticon