Mpaka ukajiuliza kwa nini mimi? Mfano ulikuwa na kazi na sasa kazi huna, unarudi nyumbani mama anaumwa, una watoto wapo shule wanahitaji pesa. Kodi ya nyumba haitoshi, kila kitu unaona kinahitaji uwajibike ili kutatua changamoto hizo.
Mabadiliko kwenye maisha huja na sintofahamu nyingi na matokeo yasiyoeleweka kabisa.
Unapopitia kipindi kama hiki ni muhimu kukaa zaidi na kutafakari mambo makuu ambayo Mungu amekutendea katika maisha yako, na huku ukiendelea kuomba zaidi akupe amani na mpenyo wa kuyavuka hayo yote inayopitiwa.

Pia kuwa na mtu sahihi ambaye unaweza kumshirikisha mambo walau akushauri juu ya kutatua changamoto hizo. Vinginevyo unaweza kujiliuza maswali mengi pasipo majibu.
"Haijalishi mambo yanayotokea au madhara yanayoweza kutupata, kikubwa ni namna tunavyoweza kupokea yale yanayotokea kwenye maisha yetu. "
Mungu hufanya njia pasipo na njia yake kupita.
Amini kipindi hicho kitapita na bado utabaki imara.
EmoticonEmoticon