Mwanaume anapenda kwa kasi ya MATAMANIO ndo maana nikasema moyo wake hupenda kama vile zilivyo MBIO za sakafuni, Mara baada ya kupata alichokuwa anakikimbilia ndipo husimama na kuangalia mbio nyingine😅😅
Wanawake wengi wanahadaika na kasi ya MAHUSIANO MAPYA na kuyapuuza ambayo tayari wanayajuwa kwa uhalisia wake, Naelewa kwa nini Wanawake WANAPENDA mahusiano MAPYA kuliko kuyahifadhi yaliyopo tayari, Mwanamke ni Mtu anayependa kubembelezwa muda wote, na ili aone amepata mtu anayempenda ni pale anapokuja Mwanaume anayembembeleza ndo maana anapoona humbembelezi na akatokea mpya anasahau kwamba HATA ALIYEKUWA NAE MWANZONI ALIWEZA KUMBEMBELEZA.
Mwanaume siraha yake wakati wa Mwanzo ni KUBEMBELEZA si anajuwa wazi Wanawake ndo mnachokikosa kwenye Maisha yenu ya Mapenzi lakini napenda mjue jambo moja;
▪RADHA YA CHUNGWA NI PALE UNAPOLIUMA AWALI BAADA YA HAPO UNALIZOEA.
Ndivyo yalivyo MAPENZI kwa aina yoyote ile tunawajibika KUTAMBUWA kwamba ALIYECHAGULIWA NA NAFSI HUYO NDO WA KUTEMBEA NAE SAMBAMBA💃💃
Mnaoruhusu akili iingilie UTASHI WA NAFSI ujue wazi UPWEKE UTAKUMALIZA wakati huo utakuwa mwingi wa mawazo, Akili inayo mengi lakini NAFSI inahitaji jambo moja tu AMANI💪
Nawasihi Wanawake;
"MTAZAME MWANAUME KWA JAMBO MOJA TU UPENDO hayo Mengine sijui Muongo, Mwingi wa Habari naMengine mnayodhania wallah niamini WANAUME WOTE TABIA ZAO ZINAFANANA kasoro yao UMPATE MWENYE UPENDO WA DHATI"
Kumuacha Mwanaume kwa wivu niamini uendako ni kama unakwenda kupewa nafasi ya mchezaji wa akiba😅😅 Maana uliyoyakimbia unakwenda kuyaona tena, Shikilia ulichonacho kuliko kikikuponyoka ukiokote, Kinaweza kutokuwa kama kilivyokuwa💯
EmoticonEmoticon