Thursday, June 4, 2020

MWANAUME ANAYEKUPENDA UTAMJUA TU...!

Tags

Mwanaume wa kweli kwako hatakuacha ujisikie mpweke. Hata kama hayupo karibu nawe atafanya mambo ambayo yatakufanya ujisikie faraja na uwepo wake kwako.
Mwanaume wa kweli kwako atakupigia simu kujua unaendeleaje, atakutumia ujumbe na kukwambia ame-miss uwepo wako.
Mwanaume wa kweli kwako hatakudanganya na wala hatakuficha mambo yake kwako.
Mwanaume wa kweli atakufanya wewe kipaumbele kwake, atakuonyesha kuwa uwepo wako anafaidi kitu fulani.
Hatakudanganya na wala hatajaribu kukubadilisha, atahakikisha siku zote u mwenye furaha na tabasamu usoni mwako.
Atakuvumilia katika mapungufu, atakurekebisha pale inapostahili.
Hatajaribu kukusema vibaya wala kukutukana, kiufupi atakuonyesha heshima ukiwa peke yako au mbele ya watu wengine.
Mwanaume wa kweli utamtambua tangu siku ya kwanza mnaanza mahusiano, usipuuze tabia ambazo anazo ambazo unahisi hautaweza kuzivumilia kwa sababu kuingia katika mahusiano na mtu asiye wa aina yako ni ‘mzigo’.


EmoticonEmoticon