TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia chama kikuu cha upinzani nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) atakuwa leo, Septemba 19, 2020, atakuwa mkoa mmoja wa Kigoma na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.
Jana, Ijumaa, Magufuli alikuwa na mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Lissu alifanya mikutano majimbo kadhaa ya Rukwa na Katavi. Leo Jumamosi, ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaonyesha Lissu atakuwa Mpanda Mjini mkoani Katavi asubuhi kisha ataingia Kigoma akianza na Jimbo la Kigoma Kaskazini atakwenda Kalimi, Buhigwe na atamalizia mkutano Kigoma Mjini saa 10 jioni.
Ratiba hiyohiyo inaonyesha, Magufuli atakuwaUvinza Mkoa wa Kigoma kisha ataingia Mkoa wa Tabora majimbo ya Kaliua na Urambo.
Hata hivyo, Magufuli bado yuko mkoani Kigoma kwa shughuli ya kiserikali iliyoanza asubuhi leo kwa kumpokea Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, aliyefanya ziara ya siku moja nchini.
Ndayishimiye amewasili Kigoma na kupokelewa na Magufuli Uwanja wa Lake Tanganyika ambapo wamezungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza uwanjani hapo kisha kwenda kuzindua Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma na baadaye kwenda kuzungumza Ikulu ndogo mkoani humo.
EmoticonEmoticon