Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Octopizzo amemtaka Rais mteule William Ruto kuihalalisha bangi pindi tu atakapokula kiapo cha kuingia ofisini kama Rais wa tano wa Kenya.
Katika video ambayo imesambazwa mitandaoni, Octopizzo anamuelezea Ruto kwamba hata kama ataona kuhalalisha bangi ni jambo gumu basi aifanye isiwe kama ni hatia kwa mtu anayepatikana naye bali liwe tu ni jambo la kawaida.
“Najua wewe ni mkristo na kwa hiyo hili gumzo huenda litakuwa gumu kidogo kwako lakini unajua bangi ni moja ya dawa ambazo ni takatifu zaidi duniani. Na amabcho nakuomba hata si kuhalalisha matumizi yake bali ni kuiweka bangi isiwe kama hatia kwa mtu anayepatikana nayo,” alisema Octopizzo.
“Juzi nilikuona ulikutana na seneta wa Delaware, huko mtu anaruhusiwa kutembea na bangi gramu 3 kwa kujivinjari tu ilmradi mtu ako na miaka 21. Hii ni biashara ya mabilioni na tunajua kuna watu serikalini wenye wanafanya biashara hiyo,” Staa huyo alisema.
EmoticonEmoticon