Wednesday, May 6, 2020

JINSI YA KUHESABU ZIKU ZA HATARI ZA KUBEBA UJAUZITO KWA MIZUNGUKO INAYOBADILIKA BADILIKA

Tags



Niliwahi kuongelea jinsi ya kuhesabu siku za hatari kwa mizunguko ya siku 28 kwa wale ambao mizunguko yao haibadiliki kwenye makala za nyuma kama hukuiona makala hiyo soma hii hapa na ujifunze jinsi ya kuhesabu mzunguko

HIZI NDIZO SIKU HATARI ZA KUBEBA MIMBA KWA WANAWAKE..
lakini kuna watu wengi ambao mizunguko yao ya miezi inatofautiana sana, labda mwezi huu siku 27 mwezi ujao siku 30.

Kama mizunguko inatofautiana kama nilivyoongea hapo juu, kama kawaida unatakiwa uangalie mzunguko wako kwa miezi sita ili uweze kujua mzunguko mrefu zaidi na mzunguko mfupi zaidi. Mfano mwezi wa kwanza mzunguko siku 30, mwezi wa pili mzunguko siku 32, mwezi wa tatu mzunguko siku 27, mwezi wa nne mzunguko siku 28, mwezi wa tano mzunguko siku 32, mwezi wa sita mzunguko siku 29.
Kwa mizunguko hiyo, mzunguko mrefu kuliko yote ni siku 32 na mzunguko mfupi kuliko yote ni siku 27. Kupata siku zako za hatari….
Mzunguko mrefu siku 32 toa 10 unapata 22.
Mzunguko mfupi siku 27 unatoa na 18 unapata 9.
Hivyo siku zako za hatari ni siku ya 9 mpaka siku ya 22 ya mwezi husika zilizobaki ni salama.
Hizo namba za kutoa yaani 10 na 18 ni costant yaani hazibadiliki , tumia kama zilivyo



EmoticonEmoticon