Wednesday, May 6, 2020

HIZI NDIO SABABU ZINAFANYA WANAWAKE WA SIKU HIZI KUOTA NDEVU NA MANYOYA AMBAYO SI YA KAWAIDA.[HIRSUTISM}

Tags



Hirsutism ni nini?
Huu ni ugonjwa ambao wanawake wanaota manyoya sehemu ambazo kikawaida wao hua hawaoti manyoya maeneo hayo mfano ndevu kidevuni, manyoya kifuani, usoni, na mgongoni wakati mwingine manyoya magumu kama ya kiume miguuni na mikononi…
Kikawaida wingi wa manyoya mwilini mwa binadamu hutegemea sana vimelea vya ukoo husika, kitaalamu kama genetics make up lakini mwanamke anapokua na manyoya mengi kama ya mwanaume hasa ndevu kuna mambo makuu mawili kwamba anaumwa au ukoo wake uko hivyo japokua waathirika wengi wa shida hii ni wagonjwa..
Dalili za ugonjwa huu ni zipi?
Mgonjwa hua na dalili za kua na manyoya mengi kama nilivyotaja hapo juu lakini pia mgonjwa huweza kua na zauti nzito kama kama mwanaume, kuota kipara, kinembe kua kikubwa, chunusi na kupungua ukubwa wa matiti..
Chanzo chake ni nini?
Mwanamke akivunja ungo huanza kutengeneza homoni za kiume na za kike ndio maana manyoya huota kwapani na maeneo ya uke hivyo homoni za kiume zikiwa nyingi kitaalamu kama adrogens mwanamke hupata hali hii ya kuota manyoya sehemu ambazo hazihusiki kama nilivyotaja hapo juu… lakini pamoja na hali hii ugonjwa huu una vyanzo vingine kama vifuatavyo.
Polycystic ovary syndrome: huu ni ugonjwa unaotokana na kutokuwa na uwiano sawa wa homoni za mwanamke kitaalamu kama homornal imbalance hivyo mwanamke hupata mzunguko wa damu ambao sio wa kawaida, kua mgumba, kunenepa na kupata uvimbe kadhaa kwenye ovari za kutengeneza mayai yake.
Matumizi ya dawa na vipodozi fulani; hii huenda ndio ikawa chanzo kikuu cha wanawake wengi kuota ndevu na manyoya kwa tabia ya kutumia dawa fulani bila maelekezo ya daktari pia siku hizi kuna maduka ya urembo yanauza dawa hizi na kuzigeuza dawa za urembo wakati ni hatari sana kiafya kwa watumiaji. kuna dawa kitaalamu zinaitwa steroids huingilia mfumo wa kiungo kinachohusika na utengenezaji wa homoni{ adrenal gland] hivyo zikitumika kwa muda mrefu huleta manyoya ambayo sio ya kawaida kwa wanawake mfano predinisolone vidonge na cream, sonaderm, candiderm,gentaline c, na dawa zingine zote zenye mchanganyiko huu kwani zipo nyingi ila mchanganyiko ni uleule ila majina tofauti ya viwanda. Dawa hizi hutakiwa zitumike kwa angalau wiki moja tu kutibu ugonjwa wa ngozi lakini wengine wamezigeuza kama mafuta ya kujipaka hivyo kama na wewe unapaka hizo aina za dawa ujue ndevu ziko njiani.
Uvimbe wa kansa;kansa za kiungo hichi kilichopo juu ya figo[adrenal gland] huongeza wingi wa homoni hizi kwenye mfumo wa binadamu na kuleta ndevu na manyoya magumu ya mwili.
Congenital adrenal hyperplasia: huu ni ugonjwa wa adrenal gland ambao mtu huzaliwa nao na kuanza kutoa homoni nyingi za uzazi na matokeo yake mtu huota ndevu na manyoya mengi mwilini..
Cushing syndrome: hali hii hutokea baada ya mgonjwa kupata matibabu ya dawa zenye homoni ya cortisol mwilini mwake kwa muda mrefu. Mfano matumizi ya dawa ya prednisolone vidonge kwa wagonjwa wa allergy na asthma.
Wakati mwingine ugonjwa huu hutokea bila sababu yeyote hasa kwa jamii za kiarabu na kihindi….
Vipimo vya kupima:
Pima kipimo kuangalia wingi wa homoni mwilini wako hasa testosterone kama zitakua zipo juu piga picha ya ultrasound ya ovary kuangalia kama kuna tatizo lolote au kupima kuangalia uvimbe wa adrenal gland mara nyingi ni moja ya vyanzo vikuu.
Matibabu
Mara nyingi kutafuta chanzo cha ugonjwa na kutibu ni moja ya matibabu bora zaidi lakini pale ambapo chanzo hakionekani dawa zifuatazo zinaweza kutumika kupunguza tatizo hilo..
malt maca; hivi ni virutubisho vinavyotengenezwa kiasili na husaidia sana kupanga homoni za uzazi katika hali ya kawaida na vimesaidia wengi, hupatikana kwa wasambazaji maalumu.
Spironolactone; hizi pia hutumika kuzuia homoni za kusababisha manyoya lakini ukitumia dawa hizi lazima utumie uzazi wa mpango kwani zinasababisha madhara makubwa sana kwa mtoto ikitokea ukibeba mimba wakati unaendelea na dozi hiyo.
Dawa za kupaka; kuna dawa inaitwa Eflornithine kitaalamu hutumika kupakwa maeneo yalioathirika na nywele nyingi kuzuia kasi ya kukua lakini hazitoi manyoya yaliyopo.
Jinsi ya kuondoa manyoya yaliyopo:
Laser therapy: hii ni miale ya mwanga ambayo inapita ndani ya ngozi kuzuia vyanzo vya ngozi{hair follicles} kuota tena mara nyingi hufanya kazi vizuri lakini gharama yake ni kubwa mno na huenda haipatikani kirahisi
Veet cream: hii ni cream inayopatikana madukani kwa bei za kawaida ukipaka inanyoa manyoya yote japokua baada ya muda yataota tena lakini inasaidia sana hasa ukipaka mara mara kwa mara au mara moja au mbili kwa wiki.
Electrolysis: hii inahusisha kuweka sindano ndogo maalumu kwa kila shimo la unywele na kuharibu chanzo chake ni moja ya matibabu mazuri ila ina maumivu makali sana na dawa za nganzi za kupakwa hutumika kupunguza maumivu hayo.
MWISHO; kama wewe ni mwanamke una ndevu au manyoya ambayo sio ya kawaida na huenda mwanzoni hayakuepo angalia kwa makini vipodozi vyako huenda ndio vinasababisha lakini pia nenda hospitali ukachunguzwe wingi wa homoni na upigwe picha ya viungo vya uzazi kama viko salama. ushauri wa bure ni kwamba serikali imekua ikipiga marufuku baadhi ya vipodozi na kuvichoma moto lakini watu wanahisi wanaonewa na kuvitafuta kwa magendo, ukiona kitu kimepigwa marufuku achana nacho ni hatari



EmoticonEmoticon