Kama umekaa kwenye mahusiano na mwanaume zaidi ya miezi sita, anafanya kazi, anaishi kwake lakini hajawahi hata siku moja kukupeleka kwake, ukimuuliza anakuambia naishi na wadogo zangu, anakupa sababu nyingine ya kijinga kabisa kuwa “Ile nyumba ina uswahili sana siwezi kukupeleka!” basi jua kuwa huyo mwanaume ameoa au ana mahusiano na mwanamke ambaye anampango wa kumuoa, anamheshimu hataki kumharibia.
Yaani hata kama huyo mwanamke haishi naye lakini hataki aje kupewa umbea kuwa jamaa alishawahi kuleta mwanamke hapa. Hataki uende kwake uache vichupi chupi vyako, vihereni na visiridia halafu mpenzi wake aje kuviona. Hivyo wewe ni mchepuko ambaye hana mpango na wewe, najua huamini kwakua unaona kama anakupenda lakini kama hujaenda kwake hata ukamsaidia kufuta vumbi kwenye madirisha basi wewe si mwanamke wake!
Lakini inawezekana ashakupelaka kwake ila huna uhuru wa kwenda kwake, huwezi kwenda unavyojisikia kama mpenzi wake mpaka umpe taarifa, ukienda bila kumuambia anakasirika na anaweza asikufungulia mlango, anaweza kuwa hata anakupiga au ukimuambia nakuja kwako kwa kushtukiza anakuambia kuwa nakuja huko, au unaweza kufika akakuambia anatoka, au kila wakati ukimpigia simu ukimuambia nakuja kwako basi anakuambia sipo nyumbani au natoka.
Huyu inawezekana hajaoa lakini ana mtu anampenda au ana michepuko mingi tu, anachotaka ni kuhakikisha anapanga ratiba zake vizuri kuhakikisha kuwa hamgongani, kwamba kila mmoja aje kwa zamu yake. Ukweli ni hivi mwanaume anayekupenda anasikia raha wewe kwenda kwake na si yeye kuja kwako, ukiona yeye ni mtu wa kuja kuja kwako lakini kwake hataki ukanyage basi jua kuwa upendo wake kwako ni watia maji tia maji, chunguza vizuri unaweza kuwa unapoteza muda wako!
EmoticonEmoticon