Saturday, May 9, 2020

USIUSEMEE MOYO 💖 WA MWINGINE JUU YA UPENDO 💞 WA DHATI WAKATI HAWEZI JAPO KUWEKEZA MUDA JUU YA UHUSIANO/NDOA YENU 📍

Tags

Upendo wa kweli Una VIGEZO VYAKE💯
Kwa vyovyote vile ili kubaini kwamba upo mahala salama YAKUPASA KUJUA UWEKEZAJI WA MWENZA WAKO KATIKA HUO UHUSIANO/NDOA mliyopo, pamoja na wewe mwenyewe kujua UNAWEKEZA NINI KWAKE? Dunia tuliyopo maana ya UPENDO inatafsiliwa vibaya, Kwa sasa ili Mtu ahisi UPENDO eti unawajibika KAMA SIO CHIMBO LAKE "wakara wa miamala" BASI UWE KIBURUDISHO CHA HAJA ZAKE ZA MWILI.
Uwekezaji muhimu kwenye UHUSIANO/NDOA ni UPENDO💞 na kinachofuata hapo ni MUDA automaticaly mengine yatazaliwa ndani ya hayo, Huwezi kuji-MWAMBAFAI UPO KWENYE PENZI TAMU huku ukijua mwenza wako hata kwenye NDOTO ZA MAISHA YAKE HAUMO ila upo kutumika kama BIG G kipindi cha KINYWA KUCHACHUKA😂😂
Watu wa sasa wametawaliwa na UBINFSI kwamba kuliko kuwa MKWELI basi yupo tayari kuugharamia UONGO ili tu akupate kwa haja zake 💯
Kuliko kujipa KIBURI kwamba unae AKUPENDAYE wakati huo wewe ni wa MPITO hesabu nafasi za ukweli ulizopewa nae, Kisha Chukuwa HATUA kuamini kwamba :-
 ANAYEKUPENDA HAWEZI KUKUFICHA HATA USHUZI WAKE
Mapenzi yenye TIJA ni yaliyo na UHURU NA UWAZI 💯 kinyume cha hapo MPO KWENYE KUTEKELEZEANA MAMBO YA NGUONI 👙
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria 🔨



EmoticonEmoticon