Sunday, May 17, 2020

Wa dada Naomba mnisamehe ila usipozingatia haya utakuja nikumbuka daima .. Listen..

Tags

Angalia umri wako na status yako saivi
Wengi mnaojitambua saivi ni mlio chuo, mmemaliza na wengine mliopo na maisha yenu najua mpo kwenye age ya 20,21,2,3,4,5,6,7,8,9,30
Age yako usidharau lakini kitu nataka kusema epuka mapenzi ya mme wa mwanamke mwezio..
Nimekutana na wadada wengi sana mpo kwenye mahusiano na wa ume za watu na mme relax na mna enjoy hamgeuki na wala hamuambiliki..
My dia hivi mwanaume anajua anapata shida sana kumfanyia interview mtu wa kumuoa
Yaani mwanaume mpaka anakuja kukuoa tambua kabisa amejilizisha mambo mengi sana kwako
Sasa mwanaume anapokuja kwako na kukutongoza ukiwa binti hujui ndoa na wewe unatarajia ndoa kwanza
Anakuja anajua kabisa kua hana sifa za kua na wewe kwa sababu tiaria ameoa kwa hiyo lazima age na gia ya
Kukujali, kukuhonga, kukutunza kukupa mtaji, kukupa unachotaka ili apate nafasi ya wewe kumsikiliza na hapo lazima utasikia anamponda mke wake ooh yule mkorofi sana
Nililazimishwa tu kumwoa baada ya kuzaa naye atasema ooh yaani hajui mapenzi kabisa yaani najua kumwoa yule mwanamke
Sasa haya maneno yatakupa kiburi na kuona kama sasa umepeta mtu na anavyokujali sasa upo lazi kumtukana kijana ambaye yupo single kisa upo na huyo mme wa mtu
My dia ccta umepotea sana na nataka nikufungue macho leo
Kama unavyowajua wanaume ni watu hawaambiliki na hawapingwi na mtu kwa nini sasa kama kweli hamupendi huyo mwanaume asimufukuze akakuoa wewe?
Kwa nini asimurudishe kwao ili akuoe wewe?
Akili yako unaipeleka wapi unashindwa kujiuliza mambo ya msingi eti unadanaganywa na wewe unakubali
Wakati mke wake ndio mwanamke pekee kati ya wanawake wote aliopita nao alimwona bora akatoa mahari akafunga ndoa akamzalisha wakajenga wakanunua gari leo wewe unadanganywa et nini nini nini na hivyo vipesa sasa unavimba mpaka unajikuta unachukua no ya mke wake unamtukana.
Hivi huelewi kwamba kama saivi upo peke yako yupo na mke wake tena kamlalia mapajani wanaangalia tv na usiku tunda la ndoa linahusika na wewe akikuona anaendelea kukupa ujinga oo jana tuligombana sana na mke wangu mpaka akazima simu ooh mara yule mshezi sana
Mdogo wangu unapotezewa muda


EmoticonEmoticon