Maneno ni bidhaa cheap ambayo mtu ni rahisi kutamka lakini matendo ni bidhaa ghali kwa sababu ni wachache hutekeleza.
Aliesema nakupenda mara nyingi sana baadae akaondoka huyo hakukupenda maana maneno yalipingana na tendo lake la kuondoka ... Aliesema anakupenda halafu akakaa na wewe siku zote huyo alikupenda kweli maana matendo yalidhihirisha.
Usiamini sana katika maneno yasioendana na vitendo maana ni rahisi kutamkika mdomoni kwa mtu.
Amini katika matendo yanayoendana na maneno anayotamka maana ametekeleza kile alichotamka.
Sehemu kubwa ya upendo ni vitendo sio maneno tu ...maneno pekee hayawezi kukufanya ukamwamini mtu maana hayawazayo moyoni mwake yawezekana asiyaseme bali akakwambia unayotaka kusikia ili uweze kufurahi lakini matendo ndio husema kweli.
Wakati mwingine ukitaka kujua tabia ya mpenzi au mchumba wako jifanye unampotezea,kumkaripia au kumuonya utajua tabia yake halisikupitia majibu na matendo yake.
Usikurupuke tu kupenda tako,sura,kifua au six pack hizo zikikosa utu wema,heshima na kujali vinakuwa kero katika mahusiano ya ndoa.
EmoticonEmoticon