Thursday, October 1, 2020

Sirro Aagiza Lissu Aripoti Polisi

Tags

 


MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amemtaka mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kuripoti kituo cha Polisi Moshi Kilimanjaro, kutokana na kitendo anachodaiwa kufanya cha kukaripia, kuwagombeza na kugombana na viongozi wa polisi.

“Nimeona viongozi wa Chadema wanakaripia askari wangu, Tundu Lissu anakaripia watu wangu, namuonya sana, jana nimeongea na Freeman Mbowe, akae azungumze na watu wake watii sheria bila shuruti.

“Lissu hayupo juu ya sheria polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na jeshi la polisi,” amesema Sirro.


EmoticonEmoticon