Thursday, October 1, 2020

Yanga Waibuka Upya! Mkataba wa Morrison & Simba Una Mapungufu

Tags

 


Klabu ya Yanga imeibua upya utata mwingine wa mkataba wa mshambuliaji Bernard Morrison wakidai hana mkataba halali na wekundu hao wa Msimbazi.

Akizungumza jioni ya Alhamis Oktoba Mosi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Frederick Mwakalebela amesema wakati klabu yao ikipokonywa haki ya umiliki wa Morrison wamebaini mapungufu makubwa katika mkataba wa mchezaji huyo na Simba.

Mwakalebela ambaye amekuja na nakala anayodai ya mkataba huo amesema sehemu zote za mkataba huo zimesainiwa na mchezaji huyo pekee hatua ambayo sio sahihi.

Amesema katika mkataba huo pia hauna sehemu iliyosainiwa na kiongozi yoyote wa bodi ya Simba lakini pia hauna saini ya shahidi.

Pia,amesema katika kila nakala imesainiwa na Morrison pekee bila ya upande wa pili hatua ambayo inaoonyesha watani wao hao hawakuridhia mkataba huo.

“Una mapungufu makubwa katika sehemu mbili…hakuwa na shahidi lakini amesaini kwenye upande wake, CEO wa Simba hajasaini. Simba SC haijaridhia mkataba wa Morrison kwa sababu hakuna sehemu yoyote ambapo klabu ya Simba imesaini mkataba wa Morrison.

FIFA inamtambua Morrison ni mchezaji wa Yanga. TMS ya FIFA inamtambua Morrison mchezaji wa Yanga. Mkabata wa Simba na Morrison una dosari, upande wa mchezaji umesainiwa bila shahidi,” – Makamu Mwenyekiti Yanga, Fredrick Mwakalebela



EmoticonEmoticon