Thursday, June 4, 2020

NI MAMBO YAPI HASA YANAYOMFANYA BINTI KUONEKANA *WIFE MATERIAL* NA KUWAVUTIA "WAOAJI" NA HATIMAYE KUOLEWA ??!....

Tags

Wanawake wengi na mabinti wamekua wakihangaika mno kutafuta namna ya kuwa na mvuto kwa wanaume WAOAJI ila wengi hufeli na kujikuta wakiangukia katika midomo ya matozi wala bata wavaa milegezo mwishowe kuishia kuchezewa na kuumizwa hisia zao. Ukweli ni kwamba kujiweka ili uonekane kuwa wewe ni WIFE MATERIAL haihitaji Degree wala Diploma.

JE! WAOAJI HUVUTIWA NA NINI ZAIDI?
Dada, Mwanaume mwenye busara hashawishiki na Uzuri ulionao, umbile lako, mawigi na mitindo ya nywele unayobadilisha kila siku, wala kwa rangi yako hiyo ya kizungu uliyoinunua dukani kwa sh 3500.

Mwanaume mwenye busara huvutiwa na Hekima, busara na maarifa uliyonayo. Uzuri wako bila Vitu hivi ni sawa na BURE, hamna kitu.
Muonekano wako wa nje utavutia wababaishaji (mashalobalo) na si Waoaji. Uzuri wako unafaa kwa matumizi ya mara moja kitandani na si kwa kuwekwa ndani.
Kweli dada ni mzuri, shape ya kuvalia Nguo unayo, hata ukivaa dela bado unaonekana, Lakini sasa unaifukuzia miaka 30 hata dalili za Ndoa hamna, unabaki kushuhudia harusi za wadogo zako miaka 20 - 22 wakiolewa.
Dada ni kweli kwa nje unaonekana mtu lakini ndani hauna kitu, upo mtupu sana, umepwaya. Haubebeki, haununuliki, wala hauuziki.
Kuna msemo usemao "Uzuri wa Mkakasi ndani kipande cha mti". Biblia pia inasema
"Mwanamke mzur asiyekuwa na HEKIMA ni sawa na Pete ya dhahabu Katika Pua ya Nguruwe" (Mithali 11 :22).
Hekima ndio kitu pekee kisichoharibika unachopaswa kujivunia nacho, hata kama bila ya Make Up, Hekima itakufanya ung'are.
"Hekima ya mtu HUMNG'ARIZA USO wake, na Ugumu wa USO wake HUBADILIKA" (Mhubiri 8 :1).
Tabia yako ndio Kikwazo chako. Mwanamke hauna nyama ya ulimi, haujui kushuka, mkali kama pilipili mbuzi kila siku hauishi Maudhi. Nani anahitaji mwanamke wa namna hii? Ni HERI ukae peke yako kwa amani kuliko kukaa na mwanamke mgomvi asiyeisha vurugu (Mithali 27 :15).
Unapenda maisha ya mtelemko, vyakula vya Supermarket kupika hautaki. Dada hivi unafikiri maisha ni movie za Kifilipino au Isidingo? Mbona una mawazo Mgando.!
Unataka mwanaume sijui mrefu, sex body, mwenye gari. Aisee, kweli..! Hekima ni ulinzi na ni zaidi ya vazi la heshima. Hilo gari Umechangia hata gharama ya kununua taili au 'site mirror'? Mbona una Vituko?
Kwa kuendekeza tamaa zisizo za msingi utatumiwa na kuachwa kama tambala la deki au Nguo ya mtumba. Nani aliyekuambia SIFA ya Mume BORA ipo kwenye kumiliki gari? Mbona unazidiwa AKILI hata Sisimizi ambaye anajua Kujitafutia?
Mwanamke mwenye busara hukubali kuanzia chini na hutafuta pamoja na Mumewe. Kuna msemo usemao UKIONA VYA ELEA, UJUE VIMEUNDWA. Na mtaka cha Uvunguni sharti Ainame.
Ngoja nikupe mfano HALISI labda utanielewa kama una kichwa cha KUELEWA. Hivi umewahi kuulizia ndoa ya Mkurugenzi wa MICROSOFT tajiri namba 1 duniani BILL GATES na mkewe aitwaye MELINDA?
Unafikiria kwanin BILL GATES alimuoa MELINDA? Ni kwa sababu ya Uzuri alionao Melinda? La hasha! Kama ni Uzuri, Bill Gates hakushindwa kuwa na mwanamke yoyote mzuri anayemtaka.
Niliwahi kusoma kwenye mtandao fulani wa kijamii kuhusu habar hii, Bill Gates alisema sababu ya kumuoa Melinda ni Hekima aliyonayo na namna anavyojua kukaa Katika nafasi yake kama Mwanamke.
Melinda alikuwa anampikia chakula yeye mwenyewe na si kutaka chakula cha supermarket, alikuwa anamfulia Nguo kwa mikono yake mwenyewe na si kwa washing machine kwa kisingizio kuwa kucha zitakatika au mikono itachubuka.
Sasa kwa huduma hizi ZOTE, ukiongezea na Uzuri alionao, kwanini Mzee asiweke chombo ndani? Hapa hakuwa na ujanja.
Sasa kama ungekuwa wewe na akili yako hiyo ya bandia, si ungeona mgodi umekudondokea. Chakula ungekuwa umeweka order ya mwaka mzima supermarket za KFC.
Nguo zingekuwa zinafuliwa India , zinaanikwa na kunyoshwa Paris Ufaransa, na zinarudishwa kwa ndege Marekani. Aisee..! Hapa upele ungempata Mkunaji.
Shika point hii ya mwisho, HAIJALISHI mwanaume awe na PESA kiasi gani, atahitaji kula chakula chako na si cha housegirl au supermarket, atahitaji kuona unamfulia Nguo zake na si kufuliwa na dobi, housegirl au washing machine.
Kuingia kwenye Ndoa TU mtihani, JE UTAWEZA kulea Mume wewe..?!
.........................................
....................
"KUMCHA MUNGU NI CHANZO CHA HEKIMA & MAARIFA "
MITHALI 1 :7.
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Usisahau ku LIKE



EmoticonEmoticon